Ni shangwe na vifijo katika kuadhimisha miezi sita ya panda digital, tuna furahia matokeo mengi chanya yaliyo tokana na Jukwaa hili. Kwa hakika Tanzania ya kidigitali inawezekana kama moja ya njia ya kutatua changamoto wanazo kumbana nazo wanawake wajasiriamali katika karne hii ya 21.
Panda digital imetatua changamoto ya ukosefu wa taarifa za fursa za mikopo, ruzuku na tuzo kwa wasichana wajasiriamali. Pia Panda Digital inatatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa wasichana kwa kuwapa ujuzi na rasilimali za kuanza na kuendesha biashara kwaajili ya kujikwamua kiuchumi.
Panda Digital imeweza kuwafikia watu wengi kwenye mikoa tofauti kama Dar es Salaam 1351, Mwanza 357, Zanzibar 33, Arusha 6 pamoja na nchi mbalimbali kama Kenya, Dublin Ireland, Lulea Sweden, USA na China.
Kwa miezi sita Panda Digital imeweza kushirikiana na Women First International Fund pamoja na Women Fund Tanzania-Trust katika kuboresha mahusiano yake na mashirika hayo. Mahusiano haya yamesaidia jukwaa la panda digital kupata ufadhili wa kuwezesha na pia kuwasaidia wasichana wajasiriamali kupata ujuzi na rasilimali za kujiajiri na kujikimu kwa lengo la kupunguza umaskini na kuwa tegemezi katika jamii.
Jukwaa la Panda Digital linatumika katika kutekeleza mradi wa Panda Digital Movement unaofanywa na Her Initiative kwa kushirikiana na Women Fund Tanzania-Trust lenye lengo la kuunda jukwaa la wanawake vijana wajasiriamali kupata ujuzi, rasilimali na uwezo kuhusiana na biashara zao. Vilevile kuanzisha na kuhamasisha mada juu ya maswala ambayo yanaathiri matarajio ya biashara zao kama rushwa za ngono, urasimishaji wa biashara, na kuhamasisha mtaji. Ili kufikia lengo hili, mradi utajibu malengo yafuatayo;
- Kuunda jukwaa moja la kusimama kwa vijana wa kike kupata ujuzi, rasilimali na fursa za kuharakisha ukuaji wa biashara ili kufikia u.
- Kujenga harakati na uwezo na kuongeza mwamko kwa wafanyabiashara vijana juu ya namna ya kujibu maswala ya rushwa za ngono.
Siku ya mtoto wa kike duniani tarehe 11 Oktoba 2021, Panda Digital ilitambuliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na shirika la Bright jamii initiative kama jukwaa la kwanza la kidigitali la kiswahili lenye lengo ya kuchochea maendeleo ya kidigitali kwa watoto wa kike kwa kuwapatia ujuzi wa kuanza na kuendesha biashara. Panda Digital ilipokea cheti cha utambuzi wa kuchochea maendeleo katika jamii kwa kumwezesha mtoto wa kike kiuchumi.
“Teknolojia imeweza kutatua changamoto tofauti tofauti wanazokutana nazo watu, tunafurahi kuona Panda Digital inaleta matokeo chanya katika kumwezesha Msichana mjasiriamali kufikia malengo yake”
~Rachel Wabanhu, Afisa Mawasiliano Her Initiative
Panda Digital imezindua kozi yake ya pili siku hii ya maadhimisho tarehe 27/10/2021 ya Muundo Biashara wa Kanvasi, kupitia kozi hii mjasiriamali anafundishwa namna ya kuunda muundo mzuri wa biashara yake ili kukidhi mahitaji ya wateja wake. Kozi hii imetolewa kwa lugha ya kiswahili kwa njia ya video ili kumsaidia kumsomaji kuelewa masomo na pia katika utelekezaji.
“Kwakweli nimeenjoy sana kozi ya masoko mtandao, nilikuwa sijui vitu vingi mno ila hii kozi imenifungua macho, masomo yote yanaeleweka vema. Asante kwa kutuwekea kozi hii ya soko la mtandao, binafsi naona nikifanyia kazi nilichojifunza nitafika mbali”
~Hope Kakwezi, CEO HK Cleaning Products
Panda Digital ni jukwaa la kwanza la kiswahili lenye lengo la kuwapatia wasichana na wanawake vijana wajasiriamali ujuzi ma rasilimali za kuanza na kuendesha biashara katika uchumi wa digitali. Baada ya janga la UVIKO 19 kumekuwa na matumizi chanya ya kidigitali kwenye sekta mbalimbali kama sekta ya afya, elimu, uchumi n.k