Her Initiative kwa kushirikiana na Serengeti bytes imezindua jukwaa la kiswahili la kidigitali linaloitwa Panda Digital leo tarehe 27 Aprili 2021. Uzinduzi huu ulifanyika kwa kutumia mkutano na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Panda Digital ni jukwaa la kwanza la kiswahili lenye lengo lakuwapatia wasichana na wanawake vijana wajasiriamali ujuzi ma rasilimali za kuanza na kuendesha biashara katika uchumi wa digitali.

Panda Digital inakusudia kuwezesha wanawake wajasiriamali kujifunza stadi ambazo zinaweza kuwasaidia kujitegemea kifedha, kutengeneza kipato, kujenga biashara, kutengeneza ajira kwa wanawake wengine na kuongeza ushiriki wa wanawake vijana katika uchumi wa digitali. Jukwaa hili pia linaangazia kuchangia kufikia malengo ya maendeleo endelevu namba 4, 5 na 8 ambayo yanaongoza usawa wa kijinsia na ukuaji wa uchumi jumuishi.

 “Wanawake wengi hawapo kwenye mtandao kwahiyo wanaume wanashiriki zaidi kuliko wanawake. Kuna haja ya kuwahamasisha wanawake kuweza kushiriki kwenye mitandao na mifumo mengine ya kidigitali” –Lydia Charles Moyo Mkurugenzi Mkuu, Her Initiative

Kwa nini tunahitaji Panda Digital? Takwimu zinaonyesha kwamba wasichana na wanawake karibu bilioni 1 wanakosa ujuzi wa kufanikiwa katika kubadilisha masoko ya kazi haraka. Pia theluthi mbili ya watu wazima milioni 750 ambao hawajui kusoma na kuandika ni wanawake, idadi ambayo haijabadilika tangu 1976. Hii inaonyesha kuwa wanawake wanahitaji kuelimishwa, wanahitaji ujuzi na ufikiaji rahisi wa rasilimali.

Panda digital imetatua vizuizi vilivyopo kama ukosefu wa elimu ya kifedha, umaskini wa muda, vizuizi vya lugha, ukosefu wa rasilimali za kujifunzia kwa wanawake wanaotoka katika mazingira duni kwani kozi hizo zinatolewa bure. Panda digital pia inaondoa kizuizi cha jiografia kwani inaweza kufikia wasichana wengi zaidi ambao wanaweza kujifunza kwa wakati wao.

Jinsi ya kujiandikisha na kuanza kutumia Jukwaa la Panda Digital; Tembelea tovuti www.pandadigital.co.tz, bonyeza kitufe cha kujiandikisha, weka maelezo yako kama inavyoonyeshwa kwenye uwanja wa usajili na utaelekezwa kwa ukurasa wa nyumbani.

Jinsi ya kupata kozi na kuanza kujifunza; baada ya kufanikiwa kujisajili, utaona menyu ya kozi. Mara tu ukibonyeza, utapelekwa mahali ambapo kozi zilizopo zimeorodheshwa. Bonyeza kozi nakisha “anza kozi” Furahiya kozi hiyo. 

Bonyeza kitufe cha fursa kupata fursa tofauti, na bonyeza kitufe cha soko kutuma biashara yako au kuona biashara zingine.

Anachohitaji mwanamke ni simu, kompyuta kibao au kompyuta ndogo, upatikanaji wa mtandao na utayari na nidhamu ya kujifunza.

 “Unaweza ukajifunza sehemu nyingi mtandaoni lakini kabla ya Panda Digital hamna sehemu unaweza kwenda kama kijana au binti wa kitanzania ukahisi uko nyumbani.” -Given Edward Mwanzilishi na Mkurugenzi mkuu, Mtabe & My Elimu.

“Uboreshaji wa digitali unabadilisha ushindani wa biashara,  na wajasiriamali wamebaki bila chaguo ila kuwa wabunifu na wavumbuzi katika biashara zao. Panda Digital inatoa elimu ambayo inawasaidia wafanyabiashara wanawake kuwa wabunifu na kuongeza mauzo.” -Michael Malya Mkurugenzi Mtendaji, Serengeti Bytes.   

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *